Aziz Andabwile Mwambalasa ametufungia mjadala wa urejeo wa Aucho, Yanga. Taarifa za Aucho zimeanza kupotea pole pole kama donge la barafu linavyoyeyuka katika ndoo ya maji. Bwamdogo amekuwa na kiwango bora sana msimu huu. Miongoni mwa watu wanaofurahia uwepo wa Folz katika korido za Jangwani ni huyu Andabwile. Chini yake Aziz amepata hadi nafasi ya kurudi Taifa Stars.
Abdul Mkeyenge ✍️…..