DAR ES SALAAM:MREMBO Jeniffer Jovin, maarufu kama Niffer, amesema wanawake wanaomiliki mali walizopata kwa jasho lao huonesha nidhamu kubwa katika matumizi ya fedha.
Niffer amesema wanawake wengi wanaomiliki magari, nyumba, au biashara zao binafsi huwa na mpangilio mzuri wa kifedha na wanajua kuweka vipaumbele.
“Ukiona mwanamke ana gari lake, nyumba yake, biashara zake huyo ana nidhamu kubwa sana na pesa. Anaweza kutenga hela kwa mpangilio,” amesema Niffer.
Akiendelea kufafanua, Niffer alisema wanawake wa aina hiyo huwa na maamuzi ya kimaendeleo katika matumizi yao.
“Lazima atasema: ‘Hii natumia kusafiri kufuata mzigo, hii nanunua kiwanja, hii najenga nyumba.’ Hawa wanawake mara nyingi hata hawana watoto, lakini wana nidhamu sana na pesa na maisha yao kwa ujumla,” ameongeza Niffer.
The post Niffer: Wanawake wenye mali zao wana nidhamu ya fedha first appeared on SpotiLEO.