DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu za Bongo, Shamsa Ford, ametoa ushauri kwa mabinti ambao hawajaolewa kufuatia video ya binti aitwaye Flora iliyosambaa mitandaoni, akieleza kwa hisia sababu zilizomfanya aimbe wimbo “Kidampa.”
Shamsa amesema alipitia video hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kuguswa na maneno ya binti huyo aliyesema amekuwa katika mahusiano kwa zaidi ya miaka mitano, akijitolea kwa kila hali kumhudumia mpenzi wake.
“Katika kutembea tembea zangu mitandaoni nimekutana na clip ya dada analia, anasema amekaa na boyfriend wake zaidi ya miaka mitano, alikuwa anampa kila kitu. Wakati mwingine alikuwa anakopa pesa kwenda kumpa mwanaume wake,” amesema Shamsa.
Akimshauri Flora na mabinti wengine walioko kwenye mahusiano, Shamsa alisisitiza umuhimu wa kujithamini na kutojihusisha kupita kiasi katika majukumu yasiyo yao.
“Unajua wanawake tukipenda huwaga vipofu, my dear. Ningependa kukwambia kitu kimoja, uliye kwenye mahusiano na boyfriend, enjoy maisha. Kila mmoja afurahie maisha yake, usijipe majukumu makubwa,” ameongeza Shamsa Ford.
The post Shamsa Ford atoa somo kwa mabinti walio kwenye mahusiano first appeared on SpotiLEO.