AHMED ALLY “MOHAMMED BAJABER TULIMSAJILI AKIWA NA MAJERAHA”
Meneja wa Idara ya Habari wa Klabu ya Simba,Ahmed Ally amethibitisha ya kwamba nyota wao Mohamed Bajaber amerejea mazoezini tayari kwa kuitumikia Klabu yao baada ya kuwa nje ya uwanja akiuguza jeraha.
Ahmed Ally amesema walimsajili mchezaji huyo akiwa na majeraha na hata alipojiunga nao Madaktari wao waliamua asitumike hadi apone vizuri ndio maana watu hawajamuona uwanjani lakini kwa sasa yupo tayari na kikosi cha Kocha Dimitar Pantev