Kocha nafikiri ameshazungumza na uongozi, anataka kufanya kazi na wachezaji wachache, naona kuna ambao anaweza kuueleza uongozi kuwa wanatakiwa kupelekwa kwa mkopo au kuuzwa ikifika Januari, anasema akiwa na wachache wanajituma zaidi pia inakuwa rahisi kwa benchi lake kuwafuatilia kuliko kuwa na wachezaji 30.
“Lakini pia ameshasema kuwa hakuna mchezaji mkubwa klabuni, kila mmoja anatakiwa kufuata utaratibu unavyotaka, kila mmoja anatakiwa kuwasikiliza waalimu na hadi sasa hana kikosi cha kwanza, yule atakayepata nafasi kwenye mchezo ujao atakuwa amefanya vizuri mazoezini na siyo vinginevyo kwa kuwa anachotaka yeye ni ubora wa mchezaji na siyo historia ya nyuma,”
— Chanzo ndani ya Simba