BAADA ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Zambia kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ 🇹🇿 itashuka dimbani leo Jumanne kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Iran 🇮🇷 kwenye Uwanja wa Shabab Al Ahli, Dubai, Falme za Kiarabu.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mataifa hayo kukutana ambapo kwa mujibu wa viwango vya ubora wa soka duniani vinavyotolewa na Fifa Tanzania inashika nafasi ya 107, huku Iran ni 21.
Tofauti hiyo kubwa ya nafasi inaifanya mechi kuwa kipimo kizito kwa vijana wa Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’. Taifa Stars na Iran zinakutana zikiwa zinatoka kupoteza mechi mbili za mwisho katika mashindano tofauti.