Kwa mara nyingine tena, Meridianbet imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuwekeza katika maendeleo ya jamii kupitia michezo, kwa kudhamini rasmi “Chanika Veteran Bonanza 2025”, tukio kubwa la michezo linalowakutanisha timu za mitaa, wachezaji chipukizi na wapenzi wa soka kutoka pembe zote za Chanika.
Kupitia udhamini huu, Meridianbet imetoa jezi, mipira na zawadi mbalimbali kwa washiriki na washindi wa bonanza hilo. Hii ni sehemu ya mpango wa kampuni wa kusaidia jamii (CSR), ambao unalenga kuinua michezo ya msingi, kuibua vipaji vipya na kukuza umoja miongoni mwa vijana kupitia burudani ya soka.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, mwakilishi wa Meridianbet alisema;
“Tunaamini michezo ni chombo cha mabadiliko. Ni njia ya kujenga nidhamu, kushirikiana na kuleta matumaini mapya. Ndiyo maana Meridianbet imeamua kuwa bega kwa bega na kamati ya Chanika Veteran Bonanza 2025, ili kuhakikisha vijana wa eneo hili wanapata nafasi ya kuonesha uwezo wao na kujiamini.”
Meridianbet pia inakuletea michezo ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Bonanza hili linatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Chanika na maeneo jirani, likiibua ushindani wa hali ya juu, na burudani michezoni. Tukio hili limekuwa zaidi ya mashindano, ni jukwaa la kukuza vipaji, kuimarisha uhusiano wa kijamii, na kukutanisha vizazi tofauti katika lengo moja la kuendeleza michezo ya ndani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya bonanza hilo alishukuru kwa niaba ya washiriki wote akisema;
“Udhamini huu wa Meridianbet umetupa nguvu mpya. Ni nadra kuona kampuni kubwa ikijitokeza kuunga mkono michezo ya jamii kwa kiwango hiki. Tunathamini sana mchango wao na tunahakikisha bonanza hili linakuwa la mfano kwa wengine.”
Meridianbet inaendelea kuwa nembo ya matumaini na maendeleo nchini, kupitia miradi mbalimbali ya kijamii inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania. Kupitia Chanika Veteran Bonanza 2025, kampuni imedhihirisha kwa vitendo kwamba michezo ni zaidi ya burudani, ni nguzo ya umoja, maendeleo na fursa.
The post MERIDIANBET YATIA NGUVU KWENYE MICHEZO, YADHAMINI “CHANIKA VETERAN BONANZA 2025”.. appeared first on Soka La Bongo.