THAILAND:MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Grand International yanayoendelea kufanyika nchini Thailand, Miss Beatrice Alex, ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa baada ya kushika nafasi ya 3 katika kipengele cha Grand Talk na nafasi ya 15 katika kipengele cha Talent.
Katika kipengele cha Talent, Beatrice alitumbuiza kwa kucheza wimbo maarufu “Chambua kama Karanga” wa msanii nguli wa muziki wa asili, Saida Karoli, na kuvutia mashabiki wengi waliokuwa wakifuatilia mashindano hayo makubwa ya kimataifa.
Beatrice, ambaye ni Miss Grand Tanzania 2025, anaendelea kuwakilisha nchi kwa umahiri na kuonyesha uwezo mkubwa katika hatua za awali za mashindano hayo, huku akiungwa mkono na Watanzania wengi kupitia mitandao ya kijamii.
Mashindano ya Miss Grand International 2025 yanatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 18, 2025, ambapo Beatrice ana nafasi kubwa ya kuingia Top 5 au hata kutwaa taji la dunia.
The post Miss Grand Tanzania ang’ara Thailand first appeared on SpotiLEO.