Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, mchezo unaofuata kwa Simba SC katika anga la kimataifa ikiwa ni CAF Champions League unatarajiwa kuchezwa ugenini.
Hii ni kete ya kwanza kimataifa kwa Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev huku wachezaji wapya wa timu hiyo ikiwa ni Neo Maema, De Reuck wakipewa angalizo kuhakikisha kwamba wanapambana kupata matokeo mazuri.
Ikumbukwe kwamba mshindi wa jumla katika mchezo huu atakwenda hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amebainisha kuwa wachezaji wote wana kazi kuelekea mchezo ujao kimataifa kuhakikisha wanaendeleza utamaduni wa timu hiyo kupata matokeo mazuri.
“Wachezaji wapya baadhi De Reuck na Maema wanaifahamu historia waliyoikuta Simba ya ushiriki wetu wa kimataifa na siyo hao pekee pia wachezaji wengine kama yupo hafahamu umuhimu wa kufuzu makundi lazima atambue na kuendeleza ile historia,”
Mchezo wa Nsingizini Hotspurs vs Simba SC ni Oktoba 19 2025 na ule wa marudiano ni Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, kwenye CAF Champions League.