Anaandika Msemaji Wa #yanga @alikamwe
Jana, Mashabiki Tulifanya jukumu letu.
Kwa mara ya kwanza, Wamalawi walishuhudia Timu ya ugenini ikiwa na mashabiki wengi Jukwaani kuliko timu yao ya nyumbani.
Hawajawahi kuona hili huko nyuma, sio mechi zao za ngazi ya Klabu tu, hata kwa Timu za Taifa, Jana ndio mara ya kwanza waliiona KLABU KUBWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI ikitamba jukwaani👊🏼
Bahati mbaya kwetu, Dakika 90 hazikuwa na furaha kwa upande wetu. Tulipoteza mchezo kwa goli 1-0 na tukaondoka wanyonge uwanjani.
Najua maumivu yetu yalivyokuwa baada ya mchezo.
Kwa wingi wetu uwanjani, kwa jinsi Mashabiki wetu walivyojitoa na kusafiri kwa umbali mrefu kutoka Tanzania hadi kufika Malawi, Matarajio yetu yalikuwa tupate Furaha jana.
Lakini ndio Football.
Dakika 90 za jana zimekwisha Lakini Sio kwamba FURAHA yetu kwenye CHAMPIONS LEAGUE msimu huu imekwisha. Bado tuna DAKIKA 90 nyingine nyumbani.
Malengo Yetu ni KUCHEZA GROUP STAGE👊🏼
Kama kuna jambo baya zaidi kwetu, ni kuendelea kuweka vichwa vyetu chini na tukaingia kwenye mtego wa kuchambua matukio ya jana, tukakwama kwenye maandalizi ya mchezo wa nyumbani.
Tusikubali hili Wananchi. tuanze sasa Maandalizi, Mtaa kwa Mtaa, Tawi kwa Tawi kuhakikisha Tunaipeleka Timu yetu GROUP STAGE.
Tuivamie hii Mechi ya Marudiano dhidi ya Silver Strikers kikubwa zaidi.
Na jambo zuri, kwenye hizi mechi za Mtoano, Jambo muhimu zaidi ni KUVUKA GROUP STAGE na sio Matokeo ya mechi moja ya ugenini.
Huzuni yetu ya jana tuigeuze kuwa msingi mkubwa wa kutupa Morali ya kufanya COME BACK ya Kibabe Jumamosi UWANJA WA MKAPA 👊🏼🔰