Nani alaumiwe? Anaweza kuwa Injinia Hersi Said mwenyewe. Yanga ilifika fainali za Shirikisho miaka ya karibuni. Yanga ilitolewa robo fainali. Yanga ilitolewa pia makundi. Hersi anajua ndoto za Wanayanga. Huwa wananyanyasika kwa mashabiki wa mtani zao kwa kutofanya vizuri katika michuano ya CAF. Ligi ya Mabingwa.
.
Wakati huu wakiwa wamesajili wachezaji wazuri huku akiendelea kumiliki wachezaji mafundi kama kina Pacome Zouzoua, Hersi akaitafutia Yanga kocha mwanafunzi. 😀
.
Ukitazama wasifu wa Folz, alikuwa amepita katika klabu kadhaa akiwa kama kocha msaidizi. Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari kwa kumleta Folz. Hajawahi kuwa kocha mkuu wala kutwaa taji lolote muhimu katika maisha yake ya mpira.
.
Unawezaje kutimiza ndoto zako ukiwa na kocha wa namna hii. Katika lugha ya mtaani ya Waingereza tunaweza kusema Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari. ‘Gambling’. Haukuwa muda wa Yanga kucheza bahati nasibu.
.
Ulikuwa muda wa wao kuwa na kocha ambaye ana uzoefu na anaweza kuishi katika falsafa zao. Matokeo yake Yanga wamejiweka katika hatari. Wameshafungwa ugenini na wageni wao wanaweza kuja na mbinu za ajabu. Injinia Hersi na wenzake ambao wanaongoza Yanga sasa hivi hawakufikiria kama wanaweza kuwa katika nafasi hii kwa sasa. Wakati wao wanaiwaza nusu fainali au fainali, tayari wapo hatarini kutofika hata makundi.
— LEGEND, Edo Kumwembe. [JicholaMwewe]
​Â