Cristiano Ronaldo ameishauri klabu yake ya Al-Nassr kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski ambaye atapatikana bila malipo mwishoni mwa msimu wa 2025-26.
Mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa na Barcelona kuhusu mustakabali wa Lewandowski, lakini inafahamika kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho akiwa Camp Nou.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amefunga mabao 105 na kusajili mabao 20 katika mechi 156 alizochezea Barcelona katika michuano yote, ikiwa ni pamoja na mabao manne katika mechi tisa msimu huu.
Atletico Madrid na vilabu vingine vya Uingereza pia vihusishwa na kumtaka mchezaji huyo.