Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions Oktoba 26,2025 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa maamuzi.
Ipo wazi kwamba katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 19 2025 Eswatini, Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Kwenye mchezo huo wa ugenini, Kibu Dennis alifunga mabao mawili na bao la ufunguzi lilifungwa na beki wa kati Wilson Nangu kwa pigo la kichwa akimalizia kona ya Maema.
Ahmed Ally, Meneje wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa huo ni mchezo muhimu na Wanasimba wanapaswa kujitokeza kwa wingi.
“Kuelekea mchezo huu tumeweka viingilio vya kitajiri. Viingilio ni Tanzanite – Tsh. 250,000, Platinum – Tsh. 150,000, VIP A – Tsh. 30,000, VIP B – Tsh. 20,000, VIP C – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000.
“Tunaamini kwamba hakuna Mwanasimba ambaye atashindwa kutoa 5,000 kushuhudia burudani kutoka kwa wachezaji wake wenye uwezo na kupata burudani. Njooni kwa wingi huu ni mtoko usije peke yako njoo na familia yako ufurahie kuipelekea Simba yako hatua ya makundi,”.