DAR ES SALAAM: BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva na mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards, Abbas Hamis, maarufu kama 20 Percent, amerudi rasmi kwenye anga la muziki.
Msanii huyo ambaye aliwahi kuteka nyoyo za mashabiki wengi kupitia nyimbo zenye ujumbe mzito wa kijamii, ameachia rasmi wimbo mpya unaoitwa “Niupendo” pamoja na video yake, hatua inayoashiria kurejea kwake kwa nguvu katika tasnia ya muziki.
Wengi wanamkumbuka 20 Percent kwa nyimbo zake zilizotikisa na bado zinasikilizwa hadi leo kama “Mama Neema”, “Tamaa Mbaya”, na nyingine nyingi ambazo zilihamasisha, kuelimisha na kuibua mjadala katika jamii kuhusu maisha ya kila siku.
The post Baada ya Ukimya Mrefu, 20 Percent Arudi na ‘Niupendo’” first appeared on SpotiLEO.








