Kiungo mshambualiaji wa klabu ya Singida Black Stars ya mkoani Singida raia wa Zambia Clatous Chama, amekuwa na kiwango bora tangu alipojiunga na klabu hiyo kwenye dirisha kubwa la usajili.
Chama anakumbukwa kufunga mabao mawili muhimu kwenye Fainali ya Kagame Cup dhidi ya Al Hilal ya Sudan, alifunga bao muhimu kwenye mchezo dhidi ya Rayon Sports ambapo Singida BS walishinda bao 1-0 wakiwa ugenini na bao kwenye mchezo dhidi ya Flambeau Du Centre ya Burundi wakitoka sare ya bao 1-1.
Chama anatazamwa kama miongoni mwa wachezaji muhimu na wazoefu sana kwenye kikosi cha Miguel Gamondi na anatazamiwa kuwa na mchango mkubwa Zaidi msimu huu.
Chama amejiunga na Singida BS akitokea katika klabu ya Yanga kama mchezaji huru huku Yanga kukiwa hakuna mchezaji yeyote aliyemfikia takwimu zake.






