LONDON: MABINGWA wateezi wa EPL Liverpool huenda wakamkosa mshambuliaji wao Alexander Isak watakapokabiliana na Brentford Jumamosi, huku timu hiyo ikitafuta kurejea kwenye njia ya ushindi baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya England.
Mshambuliaji huyo wa Sweden alipata majeraha ya nyonga katika ushindi wa mabao 5–1 dhidi ya Eintracht Frankfurt kwenye Ligi ya Mabingwa Jumatano, na Slot amesema hali yake “si mbaya sana,” lakini bado haifahamiki kuhusu Kiungo Ryan Gravenberch, ambaye alikosa mechi hiyo kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.
Liverpool wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kupoteza dhidi ya Crystal Palace, Chelsea na Manchester United. Slot amesema timu yake inapaswa kuzoea mabadiliko ya kimkakati, akibainisha kuwa wapinzani sasa wanacheza kuja kwa mtindo tofauti dhidi yao.

“Ninajaribu kuwaeleza wachezaji kuwa tofauti kubwa kabisa kati ya msimu huu na uliopita ni aina za mbinu tunazokutana nazo. Tulilazimika kujihami dhidi ya mipira mirefu 178 katika mechi saba za kwanza, na kisha kwenye mechi dhidi ya United tulilazimika kujihami mipira mirefu 59. Hiyo ni tofauti na nusu ya kwanza ya msimu uliopita.” – amesema slot
Slot aliongeza kuwa siri ya kuvunja ngome za wapinzani wanaocheza kwa kujilinda ipo kwenye ubunifu binafsi au mipira ya adhabu. Kocha huyo pia alitetea maoni yake kuhusu mbinu za Manchester United, akisema yalikuwa pongezi zaidi kwa kocha Ruben Amorim.
Slot pia alithibitisha kuwa beki Jeremie Frimpong atakosa mechi kadhaa zijazo kutokana na jeraha la misuli ya paja, huku kipa Alisson Becker akiendelea kuwa nje ya uwanja.
The post Majeraha yamuweka njiapanda Isak first appeared on SpotiLEO.






