Kama kuna mchezaji ambaye mashabiki wa Yanga wanatamani kumuona uwanjani siku ya Jumamosi katika mchezo dhidi ya Silver Strikers, basi ni Clement Mzize
Mzize anaonekana kama tumaini la Yanga katika eneo la ushambuliaji hasa baada ya washambuliaji tegemeo Prince Dube na Andy Boyeli kusuasua katika mechi iliyopita
Mzize hakucheza Malawi licha ya kuwa tayari alikuwa amepona majeraha yaliyomuwa nje kwa takribani wiki tatu
Benchi la ufundi walichukua uamuzi wa kumpumzisha ili kuhakikisha anaimarika kwa asilimia 100
Mshambuliaji huyo ambaye Yanga ililazimika ‘kuvunja benki’ kumbakisha katika dirisha lililopita la usajili, sasa anabeba matumaini ya Wananchi kuelekea mchezo wa Jumamosi ambao Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia mabao mawili ili kutinga hatua ya makundi
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa mpaka sasa wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, hakuna mchezaji majeruhi








