AGE – 49 years
LICENCE – UEFA Pro Licence
TEAMS – Amora , Cova da Piedade , Sporting CP , Primiero de Agosto , Angola National Team & Young Africans
✍️🏽Falsafa ya Msingi ya Uchezaji
Ni kocha anayeamini katika mpira wa akili( Intelligent Football ) usiotegemea nguvu au kasi tu bali ufahamu wa nafasi, mpangilio na uamuzi wa haraka wa matukio.
🎨 Mambo Makuu ya Falsafa yake
1- Balanced Tactical Football
Kushambulia kwa mpangilio mzuri, kujenga mashambulizi kupitia pasi fupi na kutumia wachezaji wa pembeni kufanya quick transition.
2- Possession with Purpose
Hapendi timu yake imiliki kwa takwimu tu bali kwa kutengeneza nafasi za maana na kimkakati.
3- Quick Transitions
Timu zake zina uwezo mkubwa wa kugeuka kutoka kulinda hadi kushambulia ndani ya sekunde chache.
4- Structured Defense
Timu iikiwa inazuia wachezaji wake wote wanashiriki kujilinda hata washambuliaji wana jukumu la kurudi nyuma pale wakati hawana mpira
5- Strategic Patience
Hataki timu yake icheze kwa vurugu ili kushinda haraka bali kwa mpangilio na kujenga utambulisho wao wa kudumu.
✍️🏽Mifumo ya Uchezaji Anayopendelea(Favorite Formations)
Pedro Gonçalves si kocha anayeshikilia mfumo mmoja pekee yaani “ dogmatic ”, Anapendelea sana mifumo mitatu.
🎨 4-2-3-1
Huu ulikuwa Mfumo wake maarufu akiwa Angola ambao lengo lake ni kutoa usawa kati ya kuzuia na kushambulia kwa kutumia viungo na washambuliaji wa pembeni.
🎨 4-3-3
Anautumia dhidi ya wapinzani wanaocheza wanaokabia sana juu ili kutoa machaguo mengi zaidi ya pasi na mapana ya uwanja kutoka nyuma kwenda mbele.
🎨 3-4-3 / 3-5-2
Huu anatumia mara nyingi wakati anataka kushambulia kwa tahadhari na kulinda matokeo zaidi. Pia anabadilika muundo na majukumu ya wachezaji kulingana na mwenendo wa mechi.
✍️🏽Vitu gani natarajia kuona akiongeza Young Africans? 🔰
1-Mabadiliko ya muundo wa ushambuliaji wenye mpangilio mzuri kutoka chini
2-Kuimarika kwa muundo wa uzuiaji kitu kinachoweza kuwalipa kwenye mechi kubwa zneye presha hasa za CAF CL .
3-Kuinua ubora kwa baadhi ya Wachezaji wa Young Africans








