Yanga chini ya Kocha wao Mpya Pedro inaweza kuja kutumia mifumo mitatu tofauti ambayo kocha huyo alikuwa akiitumia akiwa na Angola 4-4-2, 3-5-2 na pia 4-2-3-1.
Falsafa ya kocha huyo ni kuona timu yake inacheza soka la nidhamu la kuvutia, ikiwa na mipango sahihi ya kuzuia na kushambulia.
Kwenye mifumo hiyo, mfumo wa 4-2-3-1 ndio umekuwa maarufu ndani ya Yanga ukianza kutumiwa na makocha wanne tofauti kuanzia Nasreddine Nabi, Miguel Gamondi, Sead Ramovic na Hamdi Miloud.
Pedro akiwa Yanga ataanza historia mpya kwa kuwa kocha mkuu wa klabu ambapo kwenye historia ya wasifu wake kama kocha, hakuwahi kufundisha klabu na kuwa kocha mkuu, akibahatika kuwa kocha msaidizi mara mbili akizifundisha Amora na Cova da Piedade za kwao Ureno.
Akiwa na timu ya taifa ya Angola, Pedro alishinda Kombe la Cosafa mwaka jana.
ISHU YA DUBE
Kama kuna mchezaji amelaumiwa kwenye mchezo wa juzi alikuwa ni mshambuliaji Prince Dube ambaye alionekana kukosa utulivu akipoteza nafasi nyingi za kufunga tena za wazi.
Hata hivyo, baada ya hali hiyo Dube mwenyewe aligundua kuna kitu hakipo sawa na kuomba kutolewa kisha kwenda kukaa kwa majonzi kufuatia yale aliyokutana nayo ndani ya uwanja.
Wengi wamekuwa wakimlaumu Dube, lakini usahihi ni benchi la ufundi la Yanga na hata viongozi, kumsaidia mshambuliaji wao huyu kisaikolojia badala ya kushambulia kama ambavyo baadhi wanafanya.
Kocha Mabedi alionekana akiongea na mshambuliaji huyo kwa muda mrefu na ulikuwa uamizi mzuri kutuliza presha yake kutokana na yale yaliyotokea kwenye mchezo huo.
KOCHA MPYA KAZI ANAYO
Kocha mpya Pedro aliyetambulishwa kuchukua nafasi ya Romain Folz, ana kibarua kikubwa Yanga katika kufuata nyayo ama kupita mafanikio ya watangulizi wake.
Nabi aliifikisha Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo yenye miaka 90 tangu ilipoanzishwa mwaka 1935 na mbali na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili, Ngao ya Jamii na rekodi ya taifa ya kucheza mechi 49 za ligi mfululizo bila ya kupoteza, Gamondi na Hamdi na wenzake pia waliweka rekodi za kibabe Jangwani. Hata Folz aliyedumu kwa muda mfupi sana, alishinda Ngao ya Jamii tena kwa kumfunga mtani Simba.
Hii ni ishara kwamba Pedro ana kazi ya kufanya ili kuirejesha katika makali Yanga ambayo msimu huu licha ya kushinda imekuwa ikicheza soka ambalo linaacha miguno kwa mashabiki wake.
The post KWA MIFUMO HII 3 YA KIMAFIA YA KOCHA MPYA YANGA….KUNA TIMU ITAKULA TENA 5😁😁… appeared first on Soka La Bongo.




