
Haya ni maamuzi magumu ambayo yamefanywa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF ya kuachana na Hemed Morocco
Ukiacha maamuzi magumu pia wamefanya chaguo sahihi la kumchukua Miguel angel Gamondi kwenye michuano mikubwa kama ya Afcon
Kwanini Gamondi sio mwengine
1.Ni mwalimu ambaye anajua vizuri falsafa ya mpira wa Tanzania. Kitendo cha yeye kufundisha timu kama ya Yangasc itoshe kusema culture za Tanzania yuko nazo kichwani
- Kuwafahamu vizuri wachezaji wa taifa stars hususan wale ambao wanacheza ligi ya ndani. Ikumbukwe kua timu ya taifa ya Tanzania inaundwa na idadi kubwa ya wachezaji wa ndani na sio njee kwake ni kazi rahisi kuchagua kikosi.
Kama TFF wangeamua kutafuta kocha mpya ambaye anatoka nje ya nchi kwa muda huu uliosalia usingetosha kuwajua wachezaji wake vizuri
Nini kingetokea?
Kubwa ni kupangiwa wachezaji wa kuitwa kwenye kikosi hicho
Ukiacha hayo pili hata wachezaji ambao atawatumia kwenye michezo hiyo kwasababu asingeweza kuwajua vizuri wachezaji hao kwa muda mchache huu.
Lakini kwa Gamondi kama atakwenda kufeli na Stars sio swala la ugeni tena kwa wachezaji na mazingira bali ni swala la uwezo wake wa kimbinu.
The post Kocha Gamondi ni Chaguo Sahihi Kuifundisha Taifa Stars Kwa Sasa…. appeared first on Soka Tanzania.





