Pacome Zouzoua ni mchezaji muhimu zaidi katika kikosi cha Young Africans SC?
Tarehe 24 Februari 2024, Yanga waliwakaribisha CR Belouizdad kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya TotalEnergies CAF Champions League. Timu ilihitaji ushindi wa mabao manne ili kufuzu moja kwa moja. Licha ya kuwa na majeraha, Zouzoua alijituma binafsi na kusaidia Yanga kufuzu robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Tarehe 2 Desemba 2023, katika dakika ambazo mashabiki walikuwa wamekata tamaa dhidi ya Al Ahly, Zouzoua alitokea mbali na kusawazisha bao muhimu. Ilikuwa dakika ya nyota halisi kung’ara.
Mchezo dhidi ya Simba SC uliokuwa wa kuamua bingwa wa Ligi Kuu, ni stori inayojulikana. Alifunga bao na kutoa pasi ya bao (assist), Julai mwaka huu. Uwepo wake ulikuwa wa thamani isiyo na kipimo.
Katika mechi dhidi ya Silver Strikers FC nyumbani, alitengeneza mabao mawili kipindi cha kwanza. Hata baada ya kuumia, aliamua kuendelea kucheza kwa nguvu zake zote, akitambua umuhimu wake ndani ya timu.
Sitaki kuandika mengi. Inatosha kusema, kama taifa, tuna bahati kubwa kuwa na mchezaji kama Pacome Zouzoua kwenye ligi yetu.
The post Pacome Ndio Mchezaji Muhimu zaidi Katika Kikosi Cha Yanga appeared first on SOKA TANZANIA.




