DAR ES SALAAM: MAMA mzazi wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Sandra Abdul (Mama Dangote), amesema anamwombea dua mwanawe azidi kupata mafanikio katika maisha na kazi yake ya muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mama Dangote ameandika maneno yenye upendo na baraka kwa Diamond, akisisitiza kuwa anaendelea kumkabidhi kwa Mwenyezi Mungu ili amuepushe na mabaya.
“Zetu ni kukuombea dua uzidi kufanikiwa zaidi na zaidi mwanetu Naseeb Kichwa Diamond Platnumz. Mwenyezi Mungu akuepushe na mabaya yote. Aamiin Yaa Rabb,” ameandika Mama Dangote.
Diamond Platnumz, ambaye ni miongoni mwa wasanii wakubwa barani Afrika, amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa mama yake katika hatua mbalimbali za maisha na kazi yake ya muziki.
Amempa baraka na Dua baada ya kuwapa zawadi za mikufu aliodai ya dhahabu kila mmoja unaghalimu zaidi ya kiasi cha Tsh Million 10
The post Mama Dangote amuombea Diamond Platnumz mafanikio zaidi first appeared on SpotiLEO.





