NEW YORK: MWANARIADHA wa mbio za marathon kutoka Kenya, Eliud Kipchoge, amezua mjadala mkali mtandaoni baada ya kuibuka kwa video yake akiwa Jiji la New York, Marekani.
Katika klipu iliyovuma sana kwenye mitandao ya kijamii, kipenzi cha mashabiki wa riadha alionekana akitoka kwenye gari akiwa amevaa vazi la bluu la mchezo wa basketball, suruali ya njano, viatu vya bluu na koti jeupe la ngozi la rangi nyeusi.
Mavazi hayo yaliibua mjadala mkali kuhusu mitindo na ubunifu wa mavazi aliyovaa, huku wakenya wakibeza ubunifu huo wakilinganisha na mtindo maarufu wa eneo la Bonde la Ufa, ambao ni muonekano wa mavazi ya watu wanaokuwa katika kilimo.

Wakati huohuo, Kipchoge alionekana akivishwa na mawakala wawili, mmoja akiwa ameshikilia mlango wa gari na mwingine akingoja kwa nje.
Alikuwa na wasaidizi wawili, mwanamke na mwanaume, wote wakiwa wamevaa kwa mtindo wa kisasa na wenye mvuto wa kipekee lakini yeye alibaki akiwaacha wakenya wakibaki na mshangao kwa mavazi aliyovaa.
Mavazi ya Kipchoge yameendelea kuwa gumzo, huku wengi wakihisi ni ubunifu wa kisasa wa mavazi unaoonesha ushawishi wa kipekee wa mitindo akiwa huko New York.
The post Mavazi ya Eliud Kipchoge New York yazua mjadala Kenya first appeared on SpotiLEO.







