DELHI: MWANAMUZIKI maarufu wa R&B, kutoka Senegal Aliaune Damala maarufu Akon, alikusanya mamia ya mashabiki kwenye tamasha lake la India mjini Delhi, lakini tukio hilo limeacha masikitiko makubwa kwa wengi.
Wapenzi wa muziki walieleza mitandaoni kuwa shoo hiyo haikuwa na maandalizi mazuri, na walilalamika kuhusu utaratibu mbaya wa uandaaji.
Mashabiki waliokwenda kushuhudia tamasha hilo kwenye Uwanja wa Jawaharlal Nehru (JLN) walionekana kufurahishwa awali, lakini baadae walilalamika kuhusu ukosefu wa utaratibu na uzio wa kutosha wa kuonesha mwonekano wa wasanii. Baadhi walilazimika kukaa sehemu ambazo hawakuweza kumuona Akon, hali iliyowakasirisha wengi.
Mmoja wa mashabiki aliandika kwenye mtandao wa X akisema, “Nimenunua tiketi ya fedha kwenye tamasha la Akon, lakini hakuna njia ya kuangalia jukwaa kwa sababu miti na sauti vinazuia. Nilikuwa nimehudhuria tamasha la awali lilikuwa zuri lakini hili la sasa hakuna kitu.”
Mshiriki mwingine alisema, “Utaratibu wa tamasha la Akon kwa upande wa India ni wa hovyo kabisa! Niliamua kutumia almost 3,000 rupees lakini sikumuona Akon, na sehemu ya kusimama ilikuwa ndogo sana. Ni matumizi mabaya sana ya pesa yangu, nikalazimika kuangalia skrini muda wote sasa kulikuwa na umuhimumgani wa Kwenda kwenye onesho hilo.”
Akon mwenyewe alitangaza awali kuwa India ni sehemu maalum kwake, akisema: “India imenipatia mapenzi makubwa ni kama nyumbani kwa pili. Nishati, tamaduni, mashabiki… ni tofauti kabisa. Nimefurahi sana kurudi na kuonesha muziki wangu live. Tamasha hili litakuwa la kipekee tutafanya historia pamoja!”
Baada ya tamasha la Delhi, Akon atafanya shoo nyingine katika jiji la Bengaluru kesho 14 Novemba, na Mumbai ni 16 Novemba. Meneja wa tamasha, Aman Kumar, amesema, “Kurudisha Akon India ni sherehe. Hii ni usiku ambao mashabiki wamesubiri kwa hamu. Tunaahidi uzoefu wa kipekee utakaodumu kwa miaka mingi.”
The post Wahindi waishangaa shoo ya Akon kukosa utaratibu first appeared on SpotiLEO.






