AIRTEL Africa inaendelea kuandika historia katika ukuaji wa sekta ya mawasiliano barani Afrika, Matokeo yake ya nusu mwaka yanaonyesha namna Airtel ilivyopiga hatua kubwa. Kwa miezi sita iliyomalizika tarehe 30 Septemba 2025, kampuni ya mawasiliano na huduma za fedha kwa njia ya simu, Airtel imerekodi ongezeko kubwa la mapato, wateja, na matumizi ya huduma za kidijitali ikiakisi dhamira yake ya kuwaunganisha watu na kupanua ujumuishaji wa kifedha barani.
Airtel inafanya biashra katiak nchi 14, ambapo mapato ya Airtel Africa yaliongezeka kwa 24.5% na kufikia dola bilioni 2.98. Ongezeko hili limetokana kuongezeka kwa na matumizi ya huduma za data, pesa kwa njia ya mtandano yaani Airtel Money, na huduma za sauti. Kwa mara ya kwanza, data imekuwa chanzo kikubwa cha mapato, ikikua kwa 37%. Airtel Money pia imeongezeka kwa 30%, ikionyesha jinsi watu wengi sasa wanatumia simu kufanya miamala ya kifedha.
Idadi ya wateja wa Airtel Africa imefikia takribani milioni 174, ikiwa ni ongezeko la 11%. Wateja wa data wameongezeka kwa 20% hadi milioni 69.5, na watumiaji wa Airtel Money sasa ni milioni 49.8. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya simu janja, ambayo sasa yanafikia 46.8%, ikichochewa na mipango ya Airtel kusaidia watu kumiliki simu janja kwa njia ya mkopo na kuendelea kulipa kidogo kidogo. kupitia
Airtel Africa inaendelea kupanua mtandao wake. Katika kipindi hiki, imeshaongeza minara mipya zaidi ya 2,350 na kuongeza kilomita 4,000 za nyaya za fibre. Hii imeiwezesha mtandao wake kuwafikia watu kwa 81.5% katika masoko yake, huku 98.5% ya minara yake ikiwa ina teknolojia ya kisasa ya 4G. Kampuni pia inatazama uwezekano wa kuleta 5G katika maeneo yenye mahitaji makubwa ya data.
Kwa upande wa uendeshaji, kampuni inaendelea kufanya vizuri. Faida kabla ya makato (EBITDA) imeongezeka kwa 33.2% hadi dola bilioni 1.45, na faida baada ya kodi imepanda hadi dola milioni 376, kutoka milioni 79 mwaka uliopita. Hii inaonyesha usimamizi bora wa gharama na faida zilizopatikana baada ya kufanya marekebisho ya madeni.
Airtel Money imeendelea kuwa huduma muhimu sana kwa kampuni na kwa watumiaji. Katika kipindi hiki, huduma hiyo imepitisha miamala yenye thamani ya dola bilioni 193, ongezeko la karibu 36% ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kwa watu wengi barani Afrika, Airtel Money imekuwa njia rahisi na salama ya kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo, kuweka akiba na hata kupata mikopo isiyoukuwa na masharti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Africa, Sunil Taldar, anasema matokeo haya yanaonyesha matarajio makubwa ya soko la Afrika. “Ukuaji tunaouona katika matumizi ya data na simu janja pamoja na Airtel Money unaonyesha jinsi Afrika ina fursa kubwa ya kukua kidijitali,” alisema. “Tutaendelea kuboresha huduma, kuwekeza katika mtandao na kuhakikisha wateja wanapata huduma zinazokidhi mahitaji yao .”
Mafanikio ya Airtel Africa pia yanaonyesha mabadiliko mapya katika sekta ya mawasiliano. Watu wanahamia zaidi kwenye huduma za kidijitali kuliko simu za sauti pekee. Data sasa inatumika kufanya biashara, kwenye utoaji wa elimu kwa mtandao , na kuboresha maisha ya kila siku.
Airtel Africa imeongeza bajeti ya uwekezaji hadi dola milioni 900 kwa mwaka mzima. Kampuni pia inaendelea kutoa mgao na kununua baadhi ya hisa zake kama njia ya kuwapa thamani zaidi wawekezaji.
Kwa ujumla, matokeo haya ya nusu mwaka yanaonyesha jinsi Airtel Africa ilivyo sehemu muhimu ya safari ya Afrika ya kuwa bara lililounganishwa zaidi. Kila simu janja inayotumika, kila kifurushi cha data, na kila muamala wa Airtel Money ni hatua moja kuelekea mustakabali bora kwa watu wa Afrika.






.jpg)

