LAGOS: MUIGIZAJI maarufu wa filamu za Nollywood, Regina Daniels, ametoa tahadhari kali kwa mume wake wa zamani, Ned Nwoko, akidai kuwa amekuwa akimnyanyasa kwa muda mrefu.
Katika ujumbe mrefu aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Regina amedai kuwa mumewe huyo alimfanya kifungoni tangu akiwa na umri wa miaka 17, kwa sasa anapigana kwa ajili ya kupata uhuru wake.
Aidha, Regina alidai kuwa Ned Nwoko alihusika katika kujaribu kuharibu jina lake hadharani na faraghani, na kwamba anataka kuharibu maisha yake kwa kila namna. Katika ujumbe huo, pia alieleza kuwa mumewe huyo alimuingiza kwenye matumizi ya dawa hatarishi za kulevya kama ecstasy (molly) ili kumridhisha yeye binafsi.
“Niliharibu maisha yangu kwa kusema nilitumia dawa za kulevya. Wewe unajaribu kuleta uzushi. Uliniletea dawa za kulevya ecstasy (molly) ili kujifurahisha wewe,” aliandika Regina. Pia alidai kuwa Ned Nwoko anapanga kuchukua udhibiti wa watoto wao wawili kwa kuwasilisha ripoti ya udanganyifu kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.
“Kuja na ripoti ya udanganyifu kuhusu dawa za kulevya kwa sababu tu unataka kuwachukua watoto wangu ni kitu cha ajabu na kinachokupunguzia heshima yako binafsi,” aliandika Regina kwenye ujumbe wake. Hata hivyo, hadi sasa, Ned Nwoko hajajibu tuhuma hizo mpya, hali inayoongeza miale ya tetesi na mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii.
Suala hili linaendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi na wadau wa mastaa wa Nigeria, huku kila upande ukijaribu kulinda jina lake na hadhi yake.
The post Regina Daniels: Mume wangu alininyanyasa muda mrefu first appeared on SpotiLEO.




