
WAKATI straika wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele, akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2025 kwa upande wa Ligi za Ndani barani Afrika, Clement Mzize naye ameondoka na ile ya Bao Bora.
Katika hafla iliyofanyika mjini Rabat, Morocco, Mayele aliyewahi kucheza Yanga aliwapiku Mohamed Chibi (Pyramids) na Oussama Lamlaoui (RS Berkane).
Mayele alimaliza msimu wa Ligi ya Mabingwa akiwa mfungaji bora kwa mabao sita, pia timu yake ya Pyramids ikitwaa taji hilo.
“Najisikia furaha sana. Ni mara yangu ya kwanza kutwaa tuzo hii, ni jambo kubwa mno kwangu,” alisema raia huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Kwa upande wa Mzize, bao lililompa tuzo ni lile alilofunga katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa.
Mzize alipokea pasi akiwa nje ya boksi, akasogea kwa kasi, kisha kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Mazembe
The post Mayele, Mzize wang’ara tuzo za CAF, Waondoka na Tuzo appeared first on SOKA TANZANIA.





