WASHINGTON DC: MWANASOKA maarufu duniani Cristiano Ronaldo ambaye sasa anakipiga katika timu ya Al Naasr ya Saudi Arabia akiwa na mchumba wake Georgina wamekutana na kuzungumza na Raisi wa Marekani Donald Trump mambo kadhaa.
Mazungumzo hayo yamefanyika ndani ya ofisi ya Rais Ikulu ya Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ronaldo amemshukuru Rais Trump na mkewe kwa mazungumzo yao yaliyokuwa na mafanikio makubwa kwake.
“Asante Mheshimiwa Raisi kwa mwaliko wako na kwa mapokezi makubwa uliyonipa mimi na mke wangu mtarajiwa Georginagio. Kila mmoja wetu ana kitu cha maana cha kutoa niko tayari lufanya sehemu yangu tunapowatia moyo vizazi vipya kujenga maisha ya baadaye yaliyofafanuliwa na ujasiri uwajibikaji na amani ya kudumu,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Ronaldo kuwa kipenzi cha watu amezidi kudhihirishia dunia kwamba ana mchango mkubwa sana sio tu kwenye mpira ila hata kijamii hususani kwa vijana.
The post Ronaldo uso kwa uso na Trump first appeared on SpotiLEO.




