MUMBAI: MWANAMUZIKI na mtayarishaji maarufu wa muziki, AR Rahman, amesimulia kuhusu maisha yake magumu ya utotoni akisema kuwa wazazi wake waliwahi kutupwa mtaani na ndugu wa baba yake, hali iliyowalazimu kuanza upya katika mazingira magumu.
Rahman alisema baba yake alifanya kazi tatu kwa wakati mmoja ili kuipatia familia nyumba na kuwaweka salama, jambo ambalo baadaye liliharibu afya yake. Akitazama nyuma, Rahman alisema kuwa alipitia msongo mkubwa kila siku, hasa baada ya kufiwa na baba na nyanya yake akiwa na umri wa miaka tisa tu.
Rahman amesema mama yake, aliyebaki mlezi pekee, ndiye aliyempa nguvu na kumsaidia kuendelea na muziki licha ya changamoto nyingi. Rahman anasisitiza kuwa utoto wake ulijaa huzuni, msongo na mapambano, lakini pia ndiyo ulimjenga kuwa msanii anayeheshimiwa duniani leo.
The post AR Rahman: Wazazi walitelekezwa Mtaani, sikuwa sawa first appeared on SpotiLEO.






