LONDON: MENEJA wa Newcastle United Eddie Howe amesema Newcastle wanahitaji mchango mkubwa zaidi kutoka kwa mchezaji wao ghali zaidi, Nick Woltemade, huku wakijaribu kuamsha msimu wao wa Ligi Kuu England.
The Magpies wanarejea uwanjani Jumamosi dhidi ya Manchester City wakiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo, tofauti kubwa na kiwango chao kizuri walichoonesha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Woltemade, raia wa Ujerumani aliyesajiliwa kwa pauni milioni 69 kutoka Stuttgart majira ya kiangazi, alifunga magoli matano katika mechi zake nane za kwanza kwenye mashindano yote akiwa na Newcastle.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amefunga bao moja pekee kwenye mechi zake sita zilizopita za klabu, ingawa alifunga mabao matatu katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Luxembourg na Slovakia wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Howe, kiwango hicho si kibaya ukizingatia muda mdogo wa mazoezi waliokuwa nao pamoja.
“Amejitahidi sana kutekeleza kile tumekuwa tukimuomba. Alianza vizuri sana kwa magoli, na mafanikio yake kwenye mapumziko ya kimataifa yatamsaidia kujiamini. Kujiamini ni kila kitu kwa mshambuliaji wa kati. Anaweza kujivunia, lakini lazima tumtaka zaidi kwa sababu ndiye kitovu cha timu.” – alisema kocha huyo.
Shinikizo kwa Woltemade limeongezeka zaidi kutokana na kutokuwepo kwa mshambuliaji mwenzake, Yoane Wissa, aliyesajiliwa kwa pauni milioni 55 majira ya kiangazi lakini hajacheza hata dakika moja kutokana na jeraha la goti.

The post “Tunamhitaji sana Woltemade” – Eddie Howe first appeared on SpotiLEO.






