MSAFARA wa kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pedro unatarajiwa kuanza safari mapema leo Novemba 24,2025 kuelekea nchini Algeria.
Yanga SC baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ina kibarua kingine kwenye kundi B Novemba 28,2025 mchezo wa kwanza ugenini katika hatua ya makundi.
Ipo wazi kuwa ni Prince Dube alifunga bao la ushindi kwenye mchezo uliopita Uwanja wa New Amaan Complex akitumia pasi ya kiungo Mudathir Yahya.
Inatajwa kuwa Yanga SC wanahitaji kuondoka mapema ili kufanya maandalizi mazuri kwa wakati na kupata matokeo kwenye mchezo ujao.
Leo Yanga SC wataanza safari kuelekea Algeria ambapo watakwenda kukabiliana na JS Kabylie iliyotoka kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 dhidi ya vinara wa kundi A l Ahly ya Misri.



