STRASBOURG: BAADA ya kipindi kigumu Chelsea, beki wa England Ben Chilwell anajaribu kurejesha makali yake klabuni Strasbourg huku akilenga kurejea kwenye timu ya taifa kuonesha mashabiki wake na wapenzi wa soka waliomupuuza kuwa hawakuwa sahihi.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 anakiri kuwa kazi kubwa bado inamsubiri ikiwa atataka kuingia kwenye kikosi cha England kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia 2026.
Chilwell amesema kocha wa England, Thomas Tuchel, ambaye alishinda nae Ligi ya Mabingwa akiwa Chelsea mwaka 2021, amemwambia kuwa bado matumaini yake ya kimataifa hayajamalizika.
Akizungumza kabla ya mchezo wa Strasbourg dhidi ya Crystal Palace, kwenye Conference League kesho Alhamisi, Chilwell amesema: “itakuwa hadithi nzuri kiasi gani ikiwa nitaenda Kombe la Dunia baada ya kuwa kwenye ‘bomb squad’ ya Chelsea na kila mtu akinihesabu nje mwaka mmoja uliopita”.

“Kwa watu wengi, na hilo linatia motisha. Chelsea walikuwa wa kweli nami, hakuna chuki yoyote, lakini kwa hakika ego yangu inafurahia kuonesha watu fulani walikuwa hawako sahihi.” aliongeza
Matatizo ya Chilwell yalianza alipopata jeraha la misuli ya nyonga mwishoni mwa mwaka 2021. Baadaye alikosa Kombe la Dunia 2022 Qatar kutokana na jeraha la hamstring, kabla ya kupoteza nafasi yake Chelsea wakati Enzo Maresca alipochukua usukani 2024, na kuwa mmoja wa wachezaji waliowekwa kwenye kikosi kinachoitwa ‘bomb squad’ ya Blues.
“Labda watu 99 kati ya 100 wanasema, ‘Hapana, hatawezi kwenda, haiwezekani. Mini na kocha Tuchel tumezungumza tangu alipochukua mikoba ya England. Ningeweza kusema hivi imesemekana kuwa bado ndoto hii haijazimwa kabisa.” – aliongeza.
The post Chilwell atamani kurudi England first appeared on SpotiLEO.








