PARIS: MSHAMBULIAJI wa PSG na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or Ousmane Dembélé anatarajiwa uwanjani hii leo baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain kitakachokutana na Tottenham kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ulay kufuatia kupona majeraha ya mguu wa kushoto.
Dembélé hajacheza tangu alipotolewa mapema kipindi cha kwanza kwenye kichapo cha 2-1 cha PSG nyumbani dhidi ya Bayern Munich Novemba 4. Tukio lilitokea muda mfupi tu baada ya kurejea kutoka jeraha la msuli wa nyuma wa paja alilopata akiiwakilisha Ufaransa mwezi Septemba.
PSG, ambayo imekuwa ikisumbuliwa na majeraha msimu huu, bado itamkosa beki wa kulia wa Morocco Achraf Hakimi, ambaye aliumia kifundo cha mguu wa kushoto wakati wa mechi dhidi ya Bayern Munich.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana, PSG iliifunga Tottenham kwa mikwaju ya penalti kwenye UEFA Super Cup mwezi Agosti, ushindi uliowapatia Wafaransa hao taji lao la tano la mwaka 2025.
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa, PSG, kwa sasa wanashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya mechi nne, wakiwa pointi tatu nyuma ya vinara Bayern Munich.
The post Dembélé aiwahi Spurs UCL first appeared on SpotiLEO.








