Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia Uwanja wa Mkwakwani, uliopo Tanga, kutokana na kutokidhi vigezo vya matumizi ya ligi kwa sasa. Uamuzi huo umefikiwa baada ya ukaguzi uliofanyika hivi karibuni kubainisha kasoro kadhaa zinazohitaji marekebisho kabla ya uwanja kuruhusiwa kutumika tena kwenye michezo ya Ligi Kuu na mashindano mengine yanayosimamiwa na Bodi.
Kwa mujibu wa TPLB, uwanja huo utabaki kufungwa hadi pale matakwa yote ya kiufundi na kiusalama yatakapokamilishwa na kuthibitishwa na kamati husika.



