DAR ES SALAAM: MBUNIFU wa mavazi na mwanamitindo Agusta Masaki anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika onyesho kubwa la mavazi Africana Royal Elegance Collection at Wearnigeria, linalotarajiwa kufanyika nchini Nigeria kuanzia Novemba 28 hadi 302025.
Akizungumza na Spoti Leo, Agusta Masaki alisema kuwa fursa hiyo ni hatua muhimu katika safari yake ya ubunifu na pia ni heshima kubwa kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa.
“Nimefurahi sana kuonesha mkusanyiko wangu wa African Royal Elegance katika Wearnigeria2025 kupitia Agustafashion.tz. Kuanzia Dar es Salaam hadi Lagos, ninaenzi nguvu, uzuri na kujiamini kwa wanawake kote duniani,” amesema Agusta.

Amebainisha kuwa miongoni mwa mavazi atakayoyawasilisha ni yale ya asili yaliyotengenezwa kwa kutumia khanga za Kitanzania kutoka Kiwanda cha NIDA pamoja na vitenge, akilenga kuonyesha utamaduni wa Tanzania kupitia mitindo ya kisasa na ya kipekee.
Agusta ameishukuru Wear Nigeria nigeria kwa nafasi hiyo adhimu, huku akiwapongeza viongozi wa serikali kwa mazingira yenye kuleta motisha kwa wasanii na wabunifu nchini.
“Asante Wear Nigeria kwa fursa hii ya kipekee! Shukrani zangu kwa serikali yangu ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara, BASATA Nida kwa kunisapoti na Watanzania wenzangu kwa kunitia moyo nitakapoiwakilisha nchi yetu,” ameongeza.
Aidha, Agusta ametoa wito kwa vijana kuendelea kutumia vipaji vyao kujiajiri na kuitangaza Tanzania kupitia sanaa mbalimbali zikiwemo mitindo, muziki na maigizo, akisisitiza kuwa sanaa ni nyenzo muhimu ya kuitangaza nchi kimataifa.
The post Agusta Masaki kukiwasha onesho la mavazi Nigeria first appeared on SpotiLEO.





