NAIROBI: VIDEO vixen na mtumiaji maarufu wa mitandao ya kijamii kutoka Kenya, Huddah Monroe, amewahimiza wanawake kuwa makini wanapochanganya mvuto wa kimwili na mapenzi.
Katika chapisho lake kwenye Instagram leo Alhamisi, Novemba 27, 2025, Huddah ameeleza kwamba kemikali za asili mwilini zinaweza wakati mwingine kufanya watu waamini kuwa wako katika mapenzi halali, ilhali ni tamaa tu.
Huda alifafanua zaidia kwa mifano ya kisayansi alisema kuwa wakati wa mahusiano ya karibu, ubongo hutoa homoni iitwayo ‘oxytocin’, ambayo husababisha hisia kali za kujihusisha kimwili na mtu mwingine.
Huddah aliwaambia wanawake kusimama na kufikiria upya kuhusu mahusiano yao kabla ya kufanya maamuzi makubwa kuingia katika maopenzi.
Amesema kuwa homoni hizo zinaweza kupotosha mawazo ya mtu, kumfanya ajione kuwa mwenza wake ndiye anayefaa kuoana naye na kujenga mustakabali pamoja, ilhali siyo kweli.
“Wakati mwingine ‘oxytocin’ inayotolewa na ubongo wako wakati wa tendo hufanya uamini kuwa upendo wa kweli. Mwili wako unachanganya ubongo wako na kuufanya uone kuwa huyu ni mwenza wa kuzaa naye. pumzika, fikiria upya,” Huddah Monroe alieleza.
Ujumbe wa Huddah Monroe unakuja siku chache baada ya kushiriki mazungumzo aliyoyafanya na rapa maarufu kutoka Marekani, Rick Ross.
Jumatatu, Novemba 23, 2025, Huddah aliweka picha za mazungumzo yake ya moja kwa moja na Rick Ross kwenye Instagram, zikionyesha kuwa rapa huyo alianzisha mazungumzo hayo kwa ujasiri, akidai wazi kuwa yeye ni mali yake.
“You are mine,” ujumbe wa Rick Ross unasomeka.
Huddah alijibu kwa sauti ile ile, akisema, “You are mine too.”
Pia alionesha nia ya kufuata njia yake, akisema, “Nitatenda chochote unachosema kwa sababu WEWE NI BOSS.”
Hii ni baada ya Huddah kufichua nia yake ya kuoana naye, akieleza kuwa hiyo itamsaidia kuepuka na wanaume wengine.
The post Huddah Monroe: Wanawake tuwe makini wakati tunapenda first appeared on SpotiLEO.



