SIMBA imetangaza kuwa, inakusudia kukusanya kiasi cha Sh 29.5 Bilioni kwenye msimu huu wa 2025/26 kama bajeti ya klabu hiyo.
Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 13.5 kutoka bajeti ya mwaka uliopita ambayo ilikuwa ni kiasi Sh 26 Bilioni ikifanikiwa kukusanya Sh 24 Bilioni pekee ikipungukiwa sh 1.4 Bilioni.
“Kuna mambo yalitukwamisha tukashindwa kufika kwenye lengo letu la ukusanyaji ikiwemo hatua ya aliyekuwa mdhamini wetu Mbet kuvunja mkataba,” amesema Kahumbu.
“Baada ya kutuandikia barua ya kuvunja mkataba, kuna fedha ambazo tulikuwa tunatakiwa kupata kama Simba na hakutoa.
“Klabu inaendelea kupigania haki yake na tumefungua kesi ya madai mahakamani, kutafuta haki yetu na kesi inaendelea.
Akitangaza bajeti hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha Simba, Suleiman Kahumbu amesema katika bajeti hiyo ya Sh 29 Bilioni Simba inataka kutumia kiasi cha Sh 27 Bilioni.
Aidha, Kahumbu amesema endapo watafanikisha malengo ya kukusanya fedha hizo wanaweza kubaki na kiasi cha sh 1 Bilioni kwenye akaunti ya klabu hiyo.
The post PAMOJA NA KUANZA KINYONGE CAF….SIMBA ‘WATAGETI’ BIL 29 ZA MATUMIZI…. appeared first on Soka La Bongo.



