CALIFORNIA: MREMBO mwenye umri wa miaka 45 Kim Kardashian amerudi Paris mapema mwaka huu ili kutoa ushahidi kwenye kesi ya uhalifu wa silaha uliofanyika takriban muongo mmoja uliopita huku akisema kuwa hata mume wake wa zamani alikuwa na shaka kuhusu wizi huo kama umetokea kweli ama la.
Akiwa katika kipindi cha ‘The Kardashians’, Kim alizungumza kwa huzuni huku machozi yakimtoka alisema: “Mume wangu wa zamani aliniambia naigiza. ‘Niliiba na nikaigiza, tena alisema hayo mbele ya watu wengi.
Kim alisema kauli hiyo ilimuumiza sana kwani alimuamini mno mume wake wa zamani lakini hakuaminiwa lakini pia kauli hiyo iliathiri sana maisha yake.
Kim alikuwa na ndoa na Kanye, aliyekuwa na umri wa miaka 48 wakati wa wizi huo, ambapo alifungwa na kushikiliwa kwa bunduki huku watu kadhaa wakiiba zaidi ya dola milioni 10 na Mali. Walitengana miaka mitano baadaye mwaka 2021.
Alifurahi kutoa ushahidi mapema mwaka huu, kusikiliza ripoti na kuomba msamaha kutoka kwa waliohusika, na kuthibitisha kuwa kilichotokea kwake kilikuwa halisi hayakuwa maigizo kama alivyokuwa akihisiwa awali.
“Kwenda kortini na kukabiliana na watu hawa na kusikia ripoti zao na msamaha wao, ni kama kusema. Nimefurahi kuwa tumemaliza.’”
Kesi ya Mei iliwahusisha washukiwa wanane kuhukumiwa kwa makosa tofauti yanayohusiana na tukio hilo.
“Nashukuru sana kwa mamlaka za Ufaransa kwa kuendesha kesi hii. Uhalifu huo ulikuwa ni tukio la kutisha zaidi maishani mwangu, likiwa na athari ya kudumu kwangu na familia yangu.
Ingawa sitaisahau kamwe kilichotokea, naiamini nguvu ya ukuaji na uwajibikaji na naomba uponyaji kwa kila mmoja. Ninasisitiza kuendelea kupigania haki, na kuhamasisha mfumo wa sheria wa haki.”
The post Kim Kardashian alia kuhisiwa mwizi na Kanye West first appeared on SpotiLEO.





