MANCHESTER: KLABU ya Aston Villa inaonekana kama timu yenye moto zaidi kwa timu za Daraja la kati katika Ligi Kuu England kwa sasa, na Jumamosi watakuwa na kazi ya kuipima tena Arsenal katika safari yake ya kuwania ubingwa.
Mexhi hiyo inapata ladha ya kipekee kutokana na kukutana tena kwa kocha Unai Emery na Arsenal klabu iliyomfukuza mwaka 2019 baada ya kupitia mwenendo mbovu zaidi katika kipindi cha miaka 27.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amekiri ubora wa Aston Villa na kiwango cha juu walichoonesha msimu huu.

“Kwa kile (Aston Villa) wamekuwa wakifanya, namna wanavyocheza na kushinda mechi, bila shaka ni timu iliyopo kwenye kiwango bora. Tunamfahamu pia kocha wao na kazi kubwa aliyoifanya huko. Tunajua kabisa ukubwa wa majukumu ya kesho.” – amesema Arteta
Baada ya kuondoka Arsenal, Emery alirejesha hadhi yake kwa kutwaa tena Kombe la Europa League akiwa na Villarreal, kabla ya kurejea England na kuibadili Aston Villa kutoka kunusurika kushuka daraja hadi kugombea wa nafasi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu huu, Villa imeendelea kuwa ‘surprise package’ ikipanda hadi nafasi ya tatu baada ya kushinda mechi nane kati ya tisa zilizopita za ligi hiyo pendwa zaidi duniani.
Ushindi dhidi ya vinara Arsenal katika Uwanja wa Villa Park unaweza kupunguza pengo hadi pointi tatu tu na kuongeza msisimko katika mbio za ubingwa.
The post Aston Villa kuzima moto wa arsenal wikiendi hii? first appeared on SpotiLEO.








