NA MWANDISHI WETU
WAHITIMU 121 wa Chuo cha Ufundi Stadi, Furahika wametakiwa kuzingatia maadili wanapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo ili kupata fursa ya kupata ajira
Mwenyekiti wa Bodi chuo hicho, Suddy Kassim Suddy ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tabata, ametoa wito huo kwa wahitimu hao wakati wa mahafali Chuo hicho Kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.
“Maisha ni yetu mchakato ili ufanikiwe kunahitahi subira, uvumilivu na kuzingatia maadili ya kazi na kutojiingiza katika kwa vitu visivyo na maadili.
Amesema kuwa maadili katika kazi ndio msingi wa kupata fursa ya kupata ajira yenye staha.
“Msiende na mambo mawili mawili yatakayoharibu mwenendo wenu wa maisha, pia mnatakiwa kuangalia kwamba mmetoka katika familia gani, mkienda kufanya tofauti mtawaumiza wazazi wenu kwani wanamatarajio makubwa kwenu baada ya kuhitimu masomo, wakiamini mnakwenda kuwa msaada kwao,” amesema.
Ameongeza kuwa mwajiri hawezi kumuajiri mtu mwenye tabia za uzinzi, wizi na nyinginezo zisizo na maadili mema.
Kuhusu mahitaji ya chuo, hicho ikiwemo upungufu wa vifaa vya kufundishia, ikiwemo kompyuta, cherehani ameahidi kulifanyia kazi kwa kuzungumza na wadau ili kuondoa changamoto hiyo.
Naye Mkuu wa Chuo, hicho Aliko Mongele, amesema kuhitimu kwa wahitimu hao katika fani za hotel, Umeme, Bandari, air ticket, ICT, udereva na nyinginezo inatoa fursa ya kusajili wapya kwa muhula mpya utakaonza Januari.-
Ameongeza kuwa kwa muhula mpya wa Januari wataanzisha kozi mpya ya ufundi bomba na kutoa wito kwa wazazi kuwapeleka vijana wao kuweza kusoma kozi hiyo na nyinginezo ili kuachana na umasikini.
Pia muhimu wa kozi ya sekretal, Laura Matechi amesema anashukuru kufanikisha ndoto yake na sasa anaamini anakwenda kuitumia ili kufanya vema katika maisha yake na kuondokana na utegemezi.
Pia muhitimu, Moses Victor, ametoa wito kwa vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto kadhaa wajitokeze kwenye Chuo hicho ili wapate elimu bure bila malipo ingawa wanacholipi na ada ya mtihani 50,000 na fomu pekee.














