Kocha wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi ni kama haiwezi TRA United (zamani Tabora United) baada ya kuendeleza rekodi mbovu mbele ya Watoza Ushuru hao kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1 kwenye Uwanja wa KMC.
Kama hujui TRA enzi ikiwa Tabora United ndio iliyompoza Gamondi akapoteza kibarua chake akiwa Yanga iliyokubali kichapo cha mabao 3-1 ikiwa ni siku chache ilipofungwa bao 1-0 na Azam FC iliyowatibulia rekodi ya kucheza mechi nane mfululizo bila kupoteza wala kuruhusu bao lolote.
Safari hii akiwa Singida amekutana na wababe wao hao na kukubali kichapo hicho kinachokuwa cha kwanza kwa timu hiyo msimu huu katika Ligi Kuu Bara.
The post KOCHA MIGUEL GAMONDI HAIWEZI TABORA UNITED appeared first on SOKA TANZANIA.






