LIVERPOOL: MAISHA yanaenda kasi sana, ni kama Mohamed Salah yupo ndotoni hivi, lakini huu ndio ukweli mchungu ambao anakutana nao sasa.
Msimu uliopita Liverpool walimpigia magoti asaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia, Salah aliwasumbua mno hadi alipokuja kusaini mkataba huo.
Kilichompa kiburi Salah ni kiwango chake kwani alikuwa mchezaji bora wa EPL msimu uliopita na kwa Liverpool pia.
Ghafla mambo yamebadilika hatakiwi tena Anfield sababu ikiwa hajizawekwa wazi lakini yeye mwenyewe amenukuliwa akisema kila kitu kimeharibika na kuna watu wanataka kumfanya yeye kuwa mbuzi wa kafara jambo ambalo halitaki.
Fununu zinaeleza kuwa staa huyo wa Kimataifa wa Misri ameipigia familia yake simu na kuwapa taarifa kuwa waende Anfield kwenye mchezo ujao dhidi ya Brighton kwani unaweza kuwa mchezo wake wa mwisho akiwa na Liverpool licha ya kwamba hajui kama atacheza.
Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kuwa Salah amekwisha amua kuondoka Liverpool baada ya sintofahamu iliyojitokeza hivi karibuni akipigwa benchi mechi tatu mfululizo.
Taarifa hizo zinaendelea kueleza kuwa Salah hatojumuishwa kwenye kikosi cha Liverpool kitakachosafiri kuifuata Inter Milan kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ukiwa ni uamuzi wa kocha Arne Slot ambaye amegombana na Salah kwasasa.
The post Picha la Salah, Liverpool linatisha! first appeared on SpotiLEO.






