Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kitakachoshiriki fainali za mataifa ya Afrika AFCON zinazotarajia kuanza kurindima mwisho wa mwezi huu nchini Morocco.
Pacome aliitwa hivi karibuni kwenye kampeni za kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia huku akikabidhiwa jezi namba 7 mgongoni.
Wachezaji wote walioitwa Timu ya Taifa ya Ivory Coast wanacheza nje ya Bara la Afrika akiwemo Mshambuliaji wa Manchester United Amad Diallo.






