LONDON: MWANDISHI wa riwaya mashuhuri Kinsell, ambaye jina lake halisi ni Madeleine Sophie Wickham, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na ugonjwa saratani ya ubongo uliokuwa ukimsumbua aliofunguka kuwa nao mwaka 2022.
Taarifa ya kifo chake iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya Instagram usiku kuamkia leo ilisoma: “Tunasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wetu Sophie (anayejulikana pia kama Maddy, pia kama Mummy) asubuhi hii. Alifariki kwa amani, siku zake za mwisho zikiwa zimejazwa na wapendwa wake wa kweli, familia, muziki, upendo, na furaha.
“Hatuwezi kufikiria maisha yatakavyokuwa bila mng’ao wake na upendo wa maisha”. Licha ya ugonjwa wake, ambao alivumilia kwa ujasiri usiofikirika, Sophie alijihesabu kuwa amebarikiwa kweli kwa kuwa na familia bora na marafiki wazuri, lakini pia kuwa na mafanikio makubwa ya kazi yake ya uandishi. Hakupata chochote kwa urahisi na alishukuru milele kwa upendo aliopokea. “Atakumbukwa sana mioyo yetu inavunjika.”
Riwaya za Kinsella zimeuzwa nakala zaidi ya milioni 45 katika nchi zaidi ya 60, na zimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 40.
Mwaka jana, Kinsella alifichua kuwa alikuwa akipokea uthibiti wa saratani (chemotherapy) na tiba ya mionzi (radiotherapy) katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha London, na alikuwa amepitia upasuaji “uliofanikiwa”. Alisema alikuwa “akitaka kwa muda mrefu kushiriki nanyi taarifa za afya, na nimekuwa nikingojea nipate nguvu za kufanya hivyo”.
Nashukuru sana kwa familia yangu na marafiki wa karibu ambao wameniunga mkono kwa namna ya ajabu, madaktari na wauguzi wema ambao wamenitibu. Sophie ameacha mume (Henry Wickham) na watoto wa kiume wanne na binti mmoja.
The post Mwandishi nguli wa vitabu afariki dunia first appeared on SpotiLEO.






