LOS ANGELES: MUONGOZAJI filamu mashuhuri huko Hollywood ambaye aliongoza filamu ya ‘Brick’, Rian Johnson, ametetea majukwaa ya utoaji filamu mtandaoni (streaming), akieleza kuwa watu wengi hawaelewi changamoto na ugumu uliopo kati ya majumba ya sinema na kampuni za huduma za mtandao kama Netflix.
Johnson amesema: “Sio tu Netflix kusema hawatatoa filamu nyingi kwenye sinema. Kuna vita baridi kati ya Netflix na waendeshaji wa kumbi za sinema. Wengine hawatacheza filamu za Netflix kama hawatapata dirisha refu la kuonesha filamu zao.”
Amesema kuna changamoto kwa Netflix ndiyo maana wametangaza watatoa filamu chake lakini pia wanaoonesha filamu zao majumba ya sinema wanataka wanufaike nazo kabla ya kurushwa Netflix.
Johnson licha ya kutetea hayo ameijia juu AI akidai ni tishio kwa wasanii na watu wanaofanya kazi katika tasnia ya filamu.
Akihojiwa na The Hollywood Reporter, Rian alijitokeza kwa mara ya kwanza kupitia filamu yake ya mwaka 2005 ‘Brick’, iliyoshinda tuzo kwenye Tamasha la Filamu la Sundance alisema:
“AI inadhalilisha kila kitu kwa kila namna. Naelewa matumizi yake kwa mtazamo wa kuokoa pesa bila kuwalipa wasanii lakini tunakwenda wapi kama hivyo ndivyo tunataka?”
The post Netflix, Majumba ya Sinema kimeumana first appeared on SpotiLEO.







