LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA, Arne Slot amefunguka juu ya mpango wa Mohamed Salah kurejea kwenye kikosi cha Liverpool baada ya uamuzi wake wa kumpiga benchi staa huyo kuzaa matunda kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ushindi dhidi ya Inter Milan ulimshusha presha Slot shukrani kwa bao la Dominik Szoboszlai la mkwajua wa penalti kwenye dakika 88 baada ya Alessandro Bastoni kumvuta jezi Florian Wirtz.
Baada ya mechi, kocha Slot alizungumza na Mdachi mwenzake Clarence Seedorf, wakati kiungo huyo wa zamani wa Uholanzi, aliposema “kila mtu anafanya makosa”, Slot alijibu: “Umesema kila mtu anafanya makosa kwenye maisha, hivyo kitu cha kwanza kinafanywa na mchezaji aliyefanya makosa. Hilo jambo lako linapaswa litoke kwangu au kwake?”
Slot baadaye alijaribu kuelezea kwamba maneno yake hayana maana kwamba anataka Mo Salah aanze yeye kuanzisha mazungumzo ya kupata amani, aliposema: “Clarence alisema yale yalikuwa maoni yake. Sikusema kitu chochote juu ya jambo hilo, nani awe wa mwanzo au vinginevyo. Yalikuwa ni maoni yake, nimefurahi nimeweza kuelezea hilo.”
Slot alimwacha Mo Salah kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo baada ya staa huyo kufunguka kwamba amekuwa na uhusiano mbovu na kocha wake. Na kwenye hilo, Mo Salah anaamini amecheza mechi yake ya mwisho kwenye kikosi cha Liverpool kwa sababu kinachofanyika kwenye timu hiyo ni kumwondoa.
Lakini, Slot aliulizwa kama atakuwa tayari kukaa kitako na Salah kabla ya kwenda kwenye mashindano ya Afcon 2025, kocha huyo Mdachi, ambaye kikosi chake kitamenyana na Brighton uwanjani Anfield, Jumamosi, ameshindwa kutoa uhakika.
Nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk alisema: “Namfahamu Mo Salah kwa muda mrefu, tumepita mapito mengi. Amekuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Liverpool na Liverpool imekuwa sehemu kubwa ya mafanikio yake.”
Beki wa kushoto wa Andy Robertson alisema: “Chochote kinachotokea kitamalizwa ndani na ni watu
The post Vita ya Mo Salah na Kocha Arne Slot Bado Nzito Sana appeared first on SOKA TANZANIA.








