MADRID: WACHEZAJI watatu wa Real Madrid Dani Carvajal, Álvaro Carreras na Endrick wamepigwa marufuku ya mechi mbili kila mmoja kufuatia utovu wa nidhamu waliouonesha kwa waamuzi katika mechi ya LaLiga dhidi ya Celta Vigo iliyochezwa mwishoni mwa wiki.
Carreras alilimwa kadi nyekundu dakika za jioni kwenye kipigo hicho cha mabao 2-0 katika Uwanja wa Bernabéu, mchezo ambao Madrid ilimaliza wakiwa pungufu baada ya Fran García kutolewa mapema kwa kadi mbili za njano.
Endrick, ambaye hakuingia uwanjani, alitolewa nje ya uwanja kwa malalamiko kutoka benchi. Carvajal, ambaye pia hakuwa kwenye kikosi kutokana na majeraha, alidaiwa kumdhalilisha mwamuzi kwenye korido kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo.
García, ambaye alitolewa kwa kadi mbili za njano, tayari ametumikia adhabu ya mechi moja.
The post Wachezaji Madrid matatani kwa mumbughudhi refa first appeared on SpotiLEO.






