DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, William Lyimo maarufu kama Billnass, amemnunulia mke wake Faustina Mfinanga ‘Nandy’ zawadi zenye thamani ya zaidi ya Dola 20,000 za Kimarekani, sawa na takribani sh. milioni 69 za Kitanzania.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy ameposti video akionesha zawadi alizopokea kutoka kwa mume wake, jambo lililozua gumzo kubwa mitandaoni.Zawadi hizo zimeonekana kuwa za kifahari na kuvutia, zikionesha mapenzi na kuthaminiana kati ya wanandoa hao.
Miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na saa ya kifahari aina ya Rolex pamoja na pochi (handbag) ya gharama kubwa, ambazo zimevutia hisia za mashabiki na wadau wa burudani.Tukio hilo limeendelea kupongezwa na wengi, wakieleza kuwa Billnass ameonesha mfano mzuri wa kuthamini mwenza wake.
Maoni yako ni yapi? Je, ungependa mpenzi wako akupe zawadi gani ikiwa angekuwa na uwezo kama huo?
The post Billnass ampamba Nandy zawadi zaidi ya Dola 20,000 first appeared on SpotiLEO.






