Wakati ligi zikiwa zinasimama kupisha michuano ya mataifa ya Africa AFCON, ni wakati ambao klabu zinatazama ni nani wanamuhitaji kwenye kuongeza nguvu na yule wasie muhitaji katika kikosi.
Kumeibuka tetesi zikizungumza juu ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Jean Ahoua kuondoka kwenye kikosi cha timu hiyo katika dirisha dogo la usajili na kuibukia Raja Casablanca, timu ambayo inanolewa na Fadlu Davids ambae aliwahi kuwa kocha wa Simba alieagana na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.
Duru zinasema Fadlu anaihitaji huduma ya Ahoua kwenye kikosi chake cha Raja Casablanca, Jean ambae anasifika kama kwenye uchezaji mzuri kama kiungo mshambuliaji akicheza vizuri katika nafasi hiyo, lakini pia anafahamika vizuri na Fadlu kwasababu waliwah kufanya kazi pamoja.
Kocha huyo anaamini ahoua anaweza kumsaidia katika kuongeza kasi katika kikosi chake lakini pia kwenye mipira ambayo imekufa kwasababu Ahoua ni mzuri katika nafasi hiyo.
Mpaka sasa Jean amebakiwa na msimu huu mkataba wake kutamatika msimbazi ambapo kwa taarifa za ndani zinasema kuwa Simba ipo tayari kumuuza ili ifaidike na mchezaji huyo badala ya kuondoka kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kutamatika.





