Siku zinahesabika kwenda kuyashuhudia moja ya mashindano makubwa katika Bara la Afrika yanayojulika Kama TotalEnergiesAFCON (African Cup Of Nation) yatakayoanza kutimua vumbi tareh 21 Dec 2025 nchini Morocco yanayoandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Haya ndio mashindano makubwa katika uga wa Afrika ambayo ndio fahari pekee katika soka la Afrika huku yakitazamwa ulimwenguni kote, Dunia ikishudia talanta za kipekee zilizopo africa huku timu mbalimbali zikituma wawakilishi wao kusaka vipaji mahsusi.
AFCON ilianzishwa rasmi mwaka 1957, ambapo mashindano ya kwanza yalifanyika nchini Sudan, yakishirikisha timu tatu pekee. Tangu hapo, mashindano haya yamekua kwa kasi kubwa hadi kufikia timu 24 zinazoshiriki kwa sasa, na hiyo baada ya mchujo kutoka mataifa 54 ya Afrika.
Kwa miaka mingi, muundo wa AFCON umekuwa ukibadilika kulingana na ukuaji wa soka barani Afrika. Kuanzia mwaka 1968, mashindano yalianza kufanyika kila baada ya miaka miwili. Hata hivyo, kuanzia mwaka 2013, CAF iliamua kuyahamishia katika miaka ya witiri ili yasigongane na Kombe la Dunia.
Katika historia yake, AFCON imezaa nyota wakubwa wa ssoka la Afrika na kutoa jukwaa la vipaji kutambulika kimataifa. Majina makubwa kama Samuel Eto’o, Didier Drogba, Jay-Jay Okocha, George Weah, na wengine wengi, yalitumia AFCON kama daraja la kwenda kutamba duniani. Eto’o wa Cameroon ndiye mfungaji bora wa muda wote wa AFCON akiwa na magoli 18.
Kihistoria, Misri ndiyo taifa lenye mafanikio makubwa zaidi katika AFCON, likiwa limelitwaa kombe hili mara 7, zaidi ya taifa lolote barani Afrika. Mataifa mengine yenye historia kubwa katika mashindano haya ni Cameroon, Nigeria na Ghana.
AFCON pia imebeba simulizi nzito na za kihistoria. Tukio la kusikitisha zaidi ni ajali ya ndege ya timu ya taifa ya Zambia mwaka 1993, iliyogharimu maisha ya wachezaji na benchi la ufundi. Lakini kwa mshangao wa dunia, Zambia ilijijenga upya na kufika fainali za AFCON 1994 ijapokua ilipoteza mbele ya Nigeria 2:1 na kuibuka mshindi wa pili
Mashindano ya mwisho yalifanyika mwaka 2023 nchini Ivory Coast, ambapo wenyeji Ivory Coast wakasalia na kombe lao kwa kumtuliza Nigeria. Mwaka huu Afcon Itafanyika kuanzia 21 Desemba 2025 hadi 18 Januari 2026 nchini Morocco, Nasi KingBet tumekuja na kampeni kabambe ya BUTUA NA AFCON ikikupa nafasi ya kubutua mi Zawadi kama Smartphone, Routers, Iphones, Pesa Taslimu na Pikipiki mpya.
Mchongo ni kubashiri na kingbet, kwa kuanza kwa kuweka pesa katika akaunti yako kupitia airel money na katika kila Bashiri yako kuhakikisha kuna mechi walau moja ya AFCON hapo utakuwe umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinza mizawadi kutoka BUTUA NA AFCON








